Mafunzo kwa watendaji wa AMCOS yaliyolenga kuboresha ufanisi/utendaji wa kazi ili kuleta maendeleo katika vyama vya msingi yamefanyika siku mbili kuanzia leo tarehe 14 – 15/05/2024 katika ukumbi wa mikutano SHIRECU (1984) LTD. Maafisa Ushirika wamewaelimisha wajumbe wa AMCOS juu ya mada nane zilizolenga kutoa mwanga kwa watendaji hao namna bora za kuviongoza vyama vyao.
MADA ZILIZOTOLEWA
1. DHANA YA USHIRIKA
2. MIKUTANO NDANI YA CHAMA CHA USHIRIKA
3. MAADILI YA VIONGOZI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA
4. MAANDALIZI YA MPANGO MKAKATI KATIKA AMCOS
5. MADA KUHUSU UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA
6. MADA YA MIGOGORO NDANI YA VYAMA VYA USHIRIKA NA TARATIBU ZA KUITATUA
7. KUANDAA NA KUENDESHA VIKAO-MIKUTANO NDANI YA CHAMA CHA USHIRIKA
8. MADA JUU YA MAJUKUMU YA VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KATIKA KUBORESHA VYAMA VYA USHIRIKA NA KUTEKELEZA SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA NA 6. YA MWAKA 2013 PAMOJA NA KANUNI ZAKE
Aidha, Afisa Ushirika Manispaa ya Shinyanga ndg. DEOGRATIUS MOMBURI amewahimiza wajumbe juu ya umuhimu wa kutambua Dhana ya Ushirika, Maadili ya viongozi katika vyama vya Ushirika pamoja na kanuni za ushirika kwani ndio misingi imara ya kuboresha na kuleta maendeleo katika vyama na Ushirika nchini. Amewasisitiza kuzijua na kuzifanyia kazi kanuni hizo saba ambazo ni:-
1. UANACHAMA ULIO WAZI
2.UONGOZI WA KIDEMOKRASIA
3. KUSHIRIKI KWA WANACHAMA KIUCHUMI
4. CHAMA CHA USHIRIKA NI CHOMBO HURU
5. KUTOA MAFUNZO, ELIMU NA HABARI
6. USHIRIKIANO BAINA YA VYAMA VYA USHIRIKA
7. USHIRIKA KUJALI JAMII
Hata hivyo amehitimisha kwa kuwahasa wajumbe kuwa, Chama cha ushirika kikianzishwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria, na kikiwa na uongozi thabiti na watendaji wenye elimu ya kutosha pamoja na maadili mema, ikiwa ni pamoja na wanachama wenye kuwajibika, kuheshimu na kufuata Sheria ya Ushirika, kanuni za ushirika na masharti ya chama husika kitakuwa imara na endelevu na kuwezesha malengo/ madhumuni yake kufikiwa na hivyo kuwa na manufaa makubwa kwa wanachama wake na jamii inayowazunguka.