Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amewataka watendaji kuendelea kuweka maslahi ya Wanachama mbele katika utendaji wao ili kuleta manufaa ya Ushirika.
Amesema hayo alipokuwa akitembelea mabanda ya Vyama na Wadau wa Ushirika Julai 3, 2024 katika Viwanja vya Ipuli ,Tabora.
Aidha, Mrajis ametoa ushauri, mapendekezo na maagizo mbalimbali ya baadhi ya changamoto za chama pamoja na kuwapongeza kwa mafanikio yaliyopo katika vyama.
Miongoni mwa masuala aliyoelekeza kufanyika katika chama ni pamoja na kuhakikisha chama kinafanya bidii kuwa na Hati Safi, kuongeza miundombinu ya kuongeza thamani, kutangaza bidhaa za vyama, na kujifunza kutoka kwa vyama vingine.